JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MIUNDOMBINU YA KITAIFA YA UFUNGUO WA UMMA.

ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

Mfumo wa PKI

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitunga Sheria ya Miamala ya Kielektroniki mwaka 2015, ikiw ana lengo la kuhamisisha  matumizi ya vyeti vya kidigitali kwa ajili ya ukuaji wa bishara mtandao salama ana e-Serikali. Sheria hii inafafania mfumo wa kiutawala na kisheria wa kuanzishwa kwa Miundombinu ya Ufunguo wa Umma (PKI) nchini Tanzania kwa lengo la kijenga uaminifu katika mazingira ya kidgitali. Hivyo, Waziri mwenye dhamana na mausala ya TEHAMA aliiteuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwa mdhibiti wa Huduma za uidhinishaji na Mamalaka ya Uidhinishaji ya Awali. 

Ili kuhakikisha usimamizi tahbiti wa PKI ya Kitaifa (NPKI), ilionekana kuna umuhimu kutunga sera na miongozo husika.Hivyo, TCRA ilianzisha Sera ya Cheti na Taarifa ya Utendaji ya Uidhinishaji (CP & CPS) kwa ajili ya usimamizi waTanzania PKI na huduma zake.

PKI ya Tanzania ni PKI ya kimadaraja  ikiwa na myororo w auaminifu ukianzia kwa Mamlaka ya Awali ya Uidhinishaji inayoendeshwa na TCRA kwa niaba ya Serekali ya Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania.Chini ya Mamalaka ya Awali ya Uidhinishaji ya Tanzania, kuna mamalaka za uidhinishaji zilizopewa leseni na TCRA ili kutoa vyeti vya kidigitali  kwa mujibu wa Kanuni za miamala ya Kielektroniki (Huduma za Uidhinishaji) ,2024.

Muundo wa Miundombinu ya Ufunguo wa Umma ya Tanzania (Tanzania PKI) ipo katika mpangilio wa ngazi tatu zifuatazo: 

Ngazi ya 0: Mamlaka ya Awali ya Udhinishaji (nje ya mtandao) ipo katika ngazi ya juu katika mpangilio huu, hii inaifanya kuwa nanga ya Uaminifu katika Miundombino ya Kitaifa ya Ufunguo wa Umma ( Tanzania National PKI). Root CA inathibitisha safu ya Mamlaka za Uidhinishaji ambazozinafuata baada ya Mamlaka ya Awali ya Uidhinishaji.

Ngazi ya 1: Mamlaka ya Uidhinishaji inayosimama kama mamlaka ya uidhinishaji ya kati iliyoidhinishwa na Mamlaka ya Uidhinishaji ya Awali ya Tanzania katika Ngazi ya 1 ya mpangilio huu.

Ngazi ya 2: Mamlak ya Uidhinishaji inayosimama kama Mamalaka toaji ya Uidhinishaji iliyoidhinishwa na  Mamlaka y aUidhinishaji ya kati katika Ngazi ya 1 ya mpangilio huu.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!
Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Ripoti Hapa