Sera ya Cheti na Taarifa ya Utendaji ya Uidhinishaji
Hati hii inayofahamika kama CP & CPS ya TCRA inayofuatwa na Mamlaka ya Uidhinishaji ya Awali ya Tanzania pamoja na Mamlaka ya Uidhinishaji zilizopo chini yake. Ni kauli kuu ya sera inayoongoza huduma za PKI ya Tanzania na kubainisha mahitaji ya kibiashara, kisheria na kiufundi kwa ajili ya kuidhinisha, kutoa, kudhibiti, kutumia, kubatilisha na kuhuisha vyeti vya kidiijitali.
Hati hii imekusanya Sera ya Cheti (CP) na Taarifa ya Utendaji ya Uidhinishaji. Hati hii ya Mamlaka ya Awali ya Uidhinishaji ya Tanzania, inaelezea jinsi ambavyo Miundombinu ya KItaifa ya Ufunguo wa Umma unakidhi uhakiki, vidhibiti vya usalama na sera na taratibu za uendeshaji na mambo mengine yanayohusiana na wajibu na majukumu kwa mujibu wa Kanuni za Miamala ya kieelktroniki.
CP/CPS hii imeandaliwa kwa mujibu wa Kikosi Kazi cha Uhandisi wa Mtandao (IETF) RFC 3647 (Internet X.509 Sera ya Cheti na Kauli ya Utendaji ya uidhinishaji Muhimu ya Umma ya Cheti cha Miundombinu na Mfumo wa Mazoea ya Uthibitishaji)
Sera ya Cheti & Kauli ya Utendaji ya Uidhinishaji 2024 (CP & CPS)